Tunaweza kufikiri kuwa tunapita kwenye hali ngumu maishani mwetu. Lakini mara
nyingi huwa tunanung’unika tu kwa sababu hatuna nguo, fedha au chakula.
Lakini wapo watakatifu wa Bwana ambao wamepitia mateso mengi kutokana na
ushuhuda wao kwa Kristo, Bwana wetu. Ni kwa sababu walimwamini Kristo, matokeo
yake wakajikuta kwenye mateso.
Hata leo wapo Wakristo wengi duniani ambao wanateseka kutokana na imani yao
kwa Mwokozi. Lakini kwa neema ya Bwana, wameng’ang’ania imani hii.





