Monday, August 26, 2013
Saturday, August 17, 2013
Wachawi Wapigwa Kisha Waumbuliwa Waziwazi na Bwana Yesu!
Mungu anatenda kazi. Kazi ya
kueneza Injili ya Yesu Kristo si kazi nyepesi kwa sababu ushindani wake hautoki
kwa wanadamu bali ni kutoka kwenye falme za giza zinazoongozwa na mapindikizi
ya mapepo yanayoongoza majeshi kwa majeshi ya pepo wachafu.
Imeandikwa:
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya
pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (Waefeso 6:12).
Sunday, August 4, 2013
Nilipokuwa Nje ya Mwili Wangu Nilimwona Mungu, na Wafu Walio Hai!
Huu ni ushuhuda wa mtumishi wa Mungu,
Dr. Roger Mills, ambaye anaishi North Carolina kule Marekani. Hii ni sehemu tu
ya ushuhuda huo ambao ameuandika kwenye kitabu. Lakini nimeona niulete viyo
hivyo katika ufupi wake, maana naamini kuwa kuna mambo ya muhimu mengi ya
kujifunza katika sehemu hii kwa ajili ya uzima wetu wa milele katika Kristo
Yesu.
Tafadhali karibu uendelee kupokea
kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kile ambacho alimfunulia mtumishi wake kwa
ajili yangu na yako.