FREE E-BOOKS


 Namna ya Kupakua

Bofya kwenye picha ya jalada la e-book unayotaka. Kisha utafunguka ukurasa wenye kitabu hicho. Humo utaona kwenye kona ya juu kulia, maneno "Download" au alama ya mshale inayotazama chini. Bofya hapo, na e-book itapakuliwa. 

  1. Jeshi la Mungu
 
Maandiko yanasema kwamba, Mungu ameshatubariki kwa baraka zote za rohoni katika Kristo Yesu. Kwa nini basi wengi wetu bado tunahangaika na maisha na kila kitu kinaonekana kuwa ni kigumu?

Jipatie e-book hii iitwayo Jeshi la Mungu ili uweze kuona ni nini kinatakiwa kufanywa nasi ili tuweze kumiliki baraka ambazo Bwana mwenyewe alitununulia kwa kifo chake msalabani.



  2. God's Worriors
  
Hiki ni kitabu kilekile cha namba 1, yaani Jeshi la Mungu, lakini kwa lugha ya Kiingereza. Ili kukipata, bofya HAPA.


 
     3. Je, sabato ni siku katika Juma? 

Wengi wetu tumekuwa tukichanganyikiwa na swali hili. Kama maandiko yanasema kuwa Kristo ni mwisho wa sheria, je, sabato ambayo nayo ilikuwa ni sehemu ya sheria imeathiriwa vipi na kuja kwa Bwana Yesu pamoja na Agano Jipya?

Unaweza kupata majibu ya maswali haya pamoja na mengine yanayohusiana na sabato kwa kupakua e-book hii iitwayo Je, sabato ni siku katika Juma?.



     4. Kuokoka na Kuishi kwa Ushindi

Watu wengi wanasema kwamba hakuna kuokoka duniani. Wanadai kwamba mtu ataokoka baada ya kufa. Je, ukweli ni nini?

Jipatie e-book hii iitwayo Kuokoka na Kuishi kwa Ushindi ili uweze kujua ukweli wa jambo hili kutokana, si na maoni ya watu, bali na maandiko, ili usije kuwa unashikilia mambo ambayo ni maagizo ya wanadamu badala ya neno la Mungu aliye hai.



     5.  Kupata Mwenzi Kibiblia

Je, umekuwa na shauku ya kumpata mwenzi wa maisha yako? Bwana Yesu anasema kwamba kila mtu na awe na mke wake; na mume wake. Kuwa na mwenzi ni jambo la kimungu na ni mapenzi ya Mungu kila mwenye shauku hiyo apate hicho anachokitaka.

Unaweza kupata ushauri na maelekezo ya kibiblia juu ya jambo hili kwa kupakua e-book hii iitwayo Kupata Mwenzi Kibiblia.



     6.  Jiandae Kukutana na Mungu Wako

Wako baadhi ya watu ambao hawaamini kuwa kuna jehanamu ya moto au mbingu. Ushuhuda ufuatao ni wa binti anayeitwa Angelica, ambaye Bwana Yesu alimpeleka jehanamu kisha mbinguni ili akajionee mwenyewe kile ambacho Biblia inakisema.

Mbingu ni halisi na jehanamu pia. Mbinguni ni kuzuri sana; lakini jehanamu ni kubaya mno. Pakua e-book hii iitwayo Jiandae Kukutana na Mungu Wako ili uweze kujua kile kinachoendelea katika ulimwengu wa roho; hatimaye uweze kujiweka tayari kwa ujio wa nchi mpya na mbingu mpya.


7.  Shetani Anavyozuia Maombi

Huu ni ushuhuda wenye nguvu sana wa kijana ambaye tangu tumboni mwa mama yake alikuwa ni ajenti wa ibilisi. Anaeleza jinsi ambavyo shetani anazuia maombi ya Wakristo kwenye anga ili yasimfkie Mungu. Pia, anaeleza jinsi ambavyo shetani anaiba yale majibu ya maombi ambayo Mungu amewatuma malaika wake wayapeleke kwa watu wanaoomba. 

Kitabu hiki kinatufundisha nini cha kufanya ili kwamba tuweze kufanya vita vya kiroho kwa mafanikio, hivyo kupokea majibu ya maombi yetu kila wakati.

15 comments:

  1. asante sana kwa vitabu hivi...mungu akubariki sana........

    ReplyDelete
  2. Amen. Ubarikiwe na wewe pia. Endelea kumtafuta Bwana Yesu kwa bidii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ubarikiwe sana James John. Kwa kweli nimejifunza mengi sana. Mungu aendelee kukupa ufunuo zaidi. Amina!

      Delete
  3. Hakuna blog iliyowahi kunibariki kama hii na hakika mtumishi ubarikiwe sana na MUNGU aendelee kukutumia zaidi na zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante brother Michael. Ashukuriwe Mungu wetu na Jina lake lizidi kuinuliwa.

      Delete
  4. Ubarikiwe sana mtumishi unayeendesha blog hii, imekuwa baraka sana kwangu. Mungu akuzidishie baraka mara nyingi

    ReplyDelete
  5. Mungu akubariki mtumishi kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuwekea vitabu kwenye blog yako endelea hivyohivyo ili tuweze kujifunza mengi....

    ReplyDelete
  6. HUDUMA YAKO NABARIKIWA SANA NAYO, MUNGU WA MBINGUNI AZIDI KUKUINUA MTUMISHI WAKE.

    ReplyDelete
  7. Amina sana...na barikiwa mno na kukua zaidi kiroho...endelea kutusaidia kwa vitabu vingine zaidi

    ReplyDelete
  8. Ndugu hata mimi nimebarikiwa na somo la sabato.

    ReplyDelete