tag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post4557568576836628674..comments2024-03-09T08:40:11.426+03:00Comments on Yesu Ni Njia: Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 8Jameshttp://www.blogger.com/profile/17057408466635820757noreply@blogger.comBlogger5125tag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post-84075379134874252492014-06-22T00:26:31.519+03:002014-06-22T00:26:31.519+03:00nashukuru sana kwa ufafanuZi wako MUNGU akubariki ...nashukuru sana kwa ufafanuZi wako MUNGU akubariki sana john.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post-26323797234456742832014-06-21T22:39:49.398+03:002014-06-21T22:39:49.398+03:00SWALI LA KWANZA JE? MTU KUOKOKA NI MAAMUZ YA MTU M...SWALI LA KWANZA JE? MTU KUOKOKA NI MAAMUZ YA MTU MWENYEWE AU NI NEEMA YA MUNGU INAYOMJILIA NA GAFLA TU ANAACHA MAOVU?

Kuokoka ni mchanganyiko wa mambo kadhaa ingawaje mwisho wa yote, mtu mwenyewe ndiye anayehusika.

Yesu alipokuwa anaondoka duniani aliacha maagizo haya: Basi, enendeni, mkawafanye MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (Mt 28:19-20).

Wale walio ndani ya Kristo tayari wana wajibu wa lazima wa kuhubiri Injili. Ndio maana Bwana akasema:
(Eze 3:18) Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; WEWE USIMPE MAONYO, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; MTU YULE MBAYA ATAKUFA katika uovu wake; LAKINI DAMU YAKE NITAITAKA MKONONI MWAKO.

(Eze 3:19) Lakini UKIMWONYA MTU MBAYA, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali WEWE UMEJIOKOA ROHO YAKO.

Maandiko haya yanamaanisha kuwa kama mtu amehubiriwa ni wajibu wake YEYE kumkubali Kristo na wala si kwamba kuna jambo la ghafla litakalotokea. Maana ya maneno yasema kuwa TUNAOKOLEWA KWA NEEMA ni kuwa, sisi hatustahili mbele za Mungu kutokana na uasi wetu kwa Mungu aliye Mtakatifu. Lakini Yeye mwenyewe aliamua kuja kutlipia wokovu kwa mauti yake mwenyewe. Neema maana yake ni upendeleo. Kwa vile sheria ya Mungu inasema kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, lakini Yeye akaamua aibebe hiyo mauti badala ya sisi tunaohusika, basi huo ni upendeleo mkubwa (neema).

Ndipo Yesu akasema:

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu AKIISIKIA sauti yangu, NA KUUFUNGUA mlango, NITAINGIA kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. (Ufunuo 3:16).

UKIMKIRI Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, NA KUAMINI moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana, kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Waebrania 10:9-10).

.......nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; BASI CHAGUA uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako. (Kumbukumbu 30:19)

Maneno niliyoandika kwa herufi kubwa yanaonyesha jinsi ambavyo mtu mwenyewe anahusika kukubali wokovu wa Kristo.

SWALI LA PILI..! JE YESU ALIPOKUFA MSALABANI AMRI KUMI ZA MUNGU ZILIISHIA PALE KAMA SIVYO KWANINI TENA INARUHUSIWA KUSALI HATA JUMAPILI.

Amri za Mungu hazijaishia msalabani. Ndio maana Bwana Yesu akasema:

(Yoh 13:34) Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Ukiwa na upendo kwa watu, hutawafanyia kile ambacho wewe usingependa kufanyiwa – hutawakosea wazazi adabu, hutaiba, hutazini, hutadanganya, n.k.

Kuhusiana na suala la kusali jumapili, naomba uende kwenye sehemu ya FREE E-BOOKS. Download e-book inayoitwa Je, Sabato ni Siku katika Juma? Humo nimeeleza kwa kirefu sana juu ya Jumamosi na Jumapili.
Jameshttps://www.blogger.com/profile/17057408466635820757noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post-91806382077663751362014-06-20T17:58:58.588+03:002014-06-20T17:58:58.588+03:00jina langu naitwa EMMANUEL MMBAGA .......
nipo pia...jina langu naitwa EMMANUEL MMBAGA .......
nipo pia facebook natumia jina la frank mmbaga(faithfull) tafadhali nijibu .....au kama unatumia na wewe facebook njoo inbox kwangu .Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post-35715628248452336792014-06-20T17:56:05.188+03:002014-06-20T17:56:05.188+03:00ndugu james nimetokea kusoma karibia shuhuda zako ...ndugu james nimetokea kusoma karibia shuhuda zako zote saa nilikuwa na maswali mawili sijui unaweza nisaidia?
swali la kwanza je? mtu kuokoka ni maamuz ya mtu mwenyewe au ni neema ya mungu inayomjilia na gafla tu anaacha maovu?.......
swali la pili..! je yesu alipokufa msalabani amri kumi za mungu ziliishia pale kama sivyo kwanini tena inaruhusiwa kusali hata jumapili.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-6160614323715964521.post-18619910785241213332014-06-19T13:13:17.090+03:002014-06-19T13:13:17.090+03:00ubarikiweubarikiweAnonymousnoreply@blogger.com